Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Zaburi 12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Ombi la msaada wakati wa dhiki Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

2 Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

3 BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi;

4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?

5 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

6 Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.

7 Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele.

8 Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo