Zaburi 1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCKITABU CHA KWANZA Njia mbili 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. 4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya