Yobu 25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCBildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu 1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, 2 Enzi na hofu zi pamoja na Mungu; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka. 3 Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake? 4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? 5 Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake; 6 Seuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu! |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya