Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yeremia 47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Hukumu juu ya Wafilisti

1 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.

2 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.

3 Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;

4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.

5 Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikatakata?

6 Ee upanga wa BWANA, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie.

7 Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo