Kitabu hiki si kilichoandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na si sehemu ya kanoni ya Kikristo wala Tanaki ya Kiyahudi. Kinaonyeshwa kwa madhumuni ya kihistoria na ya utafiti tu. Tazama maelezo kamili Tobiti 9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCNDOA YA TOBIA Fedha zarudishwa 1 Kwa hiyo Tobia akamwita Rafaeli, akamwambia, 2 Ndugu yangu Azaria, utwae mtumishi mmoja na ngamia wawili, ukaende Rage, mji wa Umedi, 3 kwa Gabaeli, ili uniletee ile fedha; tena uje naye kwenye karamu ya arusi. Yaani, Ragueli ameapa nisiondoke mimi. 4 Ati! Baba yangu anazihesabu siku, nami nikikawia sana atahuzunika mno. 5 Hivyo Rafaeli akaondoka, akaenda akatua kwa Gabaeli, akampa ile hati. Naye akaileta ile mifuko ya fedha yenye mihuri yake, akampa. 6 Asubuhi mapema wakaondoka wote wawili wakafika kwenye karamu ya arusi; naye Gabaeli akambariki Tobia na mkewe. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya