Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kitabu hiki si kilichoandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na si sehemu ya kanoni ya Kikristo wala Tanaki ya Kiyahudi. Kinaonyeshwa kwa madhumuni ya kihistoria na ya utafiti tu. Tazama maelezo kamili

Tobiti 10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Mahangaiko ya wazazi wa Tobia

1 Huko nyuma kila siku baba yake Tobiti alikuwa akizihesabu siku; na siku za safari zilipotimia, wala hawajaja.

2 Alisema, Je! Labda wamekawilishwa? Ama labda Gabaeli amekufa, wala hakuna mtu wa kumpa fedha?

3 Akahuzunika mno.

4 Lakini mkewe akamwambia, Mwanangu amekufa; tazama, alivyokawia. Akaanza kumwombolezea, akasema.

5 Ole wangu! Mwanangu; tangu siku nilipokuachia usafiri; wewe uliye nuru ya macho yangu!

6 Tobiti akamwambia, Nyamaza, usifadhaike; yu mzima.


Tobia na Sara Waondoka Ekbatana

7 Akamwambia, Nyamaza wewe, usinidanganye, mwanangu amekufa. Naye hutoka kila siku kwenda katika njia waliyoiendea; wala hakula chakula mchana kutwa: wala hakukoma usiku kucha kumwombolezea mwanawe Tobia; hata zilipotimia zile siku kumi na nne za karamu ya arusi, ambazo Ragueli amemwapia akae huko siku hizo. Ndipo Tobia alipomwambia Ragueli, Niruhusu niende, maana baba yangu na mama yangu wanakata tamaa ya kuniona tena.

8 Lakini mkwewe akamwambia, Afadhali ukae, nami nitatuma watu kwa baba yako; nao watampasha habari zako.

9 Bali Tobia akamjibu, Sivyo kabisa; bali uniruhusu niende kwa baba yangu.

10 Kwa hiyo Ragueli akaondoka akampa mkewe Sara, na nusu ya mali zake, watumishi na ng'ombe na fedha.

11 Akawabariki, akawaruhusu, akasema, Wanangu, Mungu wa mbinguni akujalieni uheri kabla sijafa.

12 Akamwambia binti yake, Waheshimu wakwezo, walio sasa kama wazazi wako; ili nipate sifa zako njema. Akambusu. Edna naye akamwambia Tobia, Ndugu yangu mpenzi, Mungu wa mbinguni akurudishe, na anijalie kuwaona watoto wako atakaokuzalia binti yangu Sara, ili nifurahi mbele za BWANA. Angalia, nimekukabidhi binti yangu amana bora, maana usimchokoze.

13 Baada ya hayo Tobia akaenda zake, hali akimhimidi Mungu kwa kuwa ameifanikisha safari yake. Akawabariki Ragueli na mkewe Edna.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo