Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Waimbaji wa hekaluni

1 Tena Daudi na makamanda wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi kulingana na utumishi wao;

2 wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.

3 Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA.

4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

5 hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

7 Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa mastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.

8 Wakapigiwa kura ya huduma zao, kwa pamoja, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

9 Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;

10 ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

11 ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

12 ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

13 ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

14 ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

15 ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

16 ya tisa Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;

17 ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

18 ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

19 ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

20 ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

21 ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

22 ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

23 ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

24 ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

25 ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

26 ya kumi na tisa Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

27 ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

28 ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

29 ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

30 ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

31 ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo