Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA alipokuwa akipita akamwona nitu, kipofu tangu kuzaliwa.

2 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Rabbi, ni nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hatta akazaliwa kipofu?

3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe kwake.

4 Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.

5 Maadam nipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.

6 Alipokwisha kusema haya, akatema mate chini, akafanya tope kwa yale mate,

7 akampaka kipofu macho kwa lile tope, akamwambia, Enenda, kanawe katika birika ya Siloam (tafsiri yake, Aliyetumwa). Bassi akaenda, akanawa, akarudi, anaona.

8 Bassi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni kipofu, wakanena, Je! huyu siye yule aliyekuwa akiomba, ameketi?

9 Wengine wakimena, Amefanana nae.

10 Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. Bassi wakamwambia, Macho yako yalifumhuliwaje?

11 Yeye akajibu, akanena, Mtu aitwae Yesu alifanya tope, akanipaka macho yangu, akaniambia, Enenda hatta birika ya Siloam, ukanawe; bassi nikaenda nikanawa, nikapata kuona.

12 Wakamwambia, Yuko wapi mtu huyo? Akanena, Sijui.

13 Wakampeleka yule aliyekuwa kipofu zamani kwa Mafarisayo.

14 Na ilikuwa sabato hapo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho.

15 Bassi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi alivyopata kuona. Akawaambia, Alitia tope juu ya macho yangu nikanawa, na sasa naona.

16 Bassi baadhi ya Mafarisayo wakanena, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakanena, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?

17 Kukawa matangukano kati yao. Bassi wakamwambia yule kipofu marra ya pili, Wewe unasema nini katika khabari zake kwa kuwa alikufumbua macho? Akasema, Yu nabii.

18 Bassi Wayahudi hawakusadiki khabari zake ya kuwa alikuwa kipofu akapata kuona, hatta wakawaita wazazi wake yule aliyepata kuona; wakawauliza, wakinena,

19 Huyu ndiye mwana wenu msemae kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, bassi, kuona sasa?

20 Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ni mwana wetu, na ya kuwa alizaliwa kipofu;

21 lakiui jinsi aonavyo sasa, hatujui, na ni nani aliyemfumbua macho, hatujui; yeye ni mtu mzima; mwulizeni yeye mwenyewe, atajisemea.

22 Wazazi wake waliyasema haya kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi wamekwisha kuwafikana kwamba mtu akimwungama kuwa Kristo, ataharamishwa sunagogi.

23 Ndio sababu wazazi wake walisema, Yeye ni mtu mzima, mwulizeni.

24 Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.

25 Bassi yule mtu akajibu akasema, Kwamba yeye m mwenye dhambi, sijui. Najua neno moja, mimi nalikuwa kipofu, na sasa naona.

26 Wakamwambia tena, Alikutenda nini? Alikufumbuaje macho?

27 Akawajibu, Nimekwisha kuwaambieni, wala hamkusikia: Mbona mnataka kusikia marra ya pili? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?

28 Bassi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake mtu yule; sisi tu wanafunzi wa Musa.

29 Sisi twajua ya kuwa Mungu alisema na Musa, bali huyo hatujui atokako.

30 Yule mtu akajibu akawaambia, Neno hili ni la ajabu, kwamba ninyi hamjui atokako, nae alinifumbua macho.

31 Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia.

32 Tangu awali haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu aliyezaliwa hali hii.

33 Kama huyu asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno.

34 Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje.

35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; akamwona, akasema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?

36 Nae akajibu, akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?

37 Yesu akamwambia, Umemwona, na yeye anaesema nawe ndiye.

38 Akasema, Naamini, Bwana; akamsujudia.

39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, illi wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.

40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu?

41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema Twaona; bassi dhambi yenu inakaa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo