Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 lakini Yesu akaenda mlima wa mizeituni.

2 Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha.

3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati,

4 wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Bassi katika torati Musa alituamuru kuwapiga mawe watu kama hao; bassi wewe wasema nini?

6 Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi.

7 Nao wakazidi kumhoji, akajiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika inchi.

9 Nao, waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianza tangu wazee hatta wa mwisho; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke akisimama katikati.

10 Yesu akajiinua asimwone mtu illa yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Hapana aliyekuhukumu?

11 Akamwambia, Hapana Bwana. Yesu akamwambia, Nami sikuhukumu. Enenda, wala usitende dhambi tena.

12 Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

13 Bassi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia nafsi yako; ushuhuda wako si kweli.

14 Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako.

15 Ninyi mwahukumu kwa jinsi ya kiwiliwili; mimi simhukumu mtu.

16 Na nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli, kwa kuwa mimi si peke yangu bali mimi na Baba aliyenipeleka.

17 Na tena katika sharia yenu imeandikwa, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli.

18 Mimi ndimi ninaejishuhudia nafsi yangu, nae Baba aliyenipeleka ananishuhudia.

19 Bassi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngaliuijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.

20 Maneno haya aliyasema Yesu akifundisha kakika hekalu, katika chumba cha hazina; wala hapana mtu aliyemkamata, kwa kuwa saa yake ilikuwa haijaja bado.

21 Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.

22 Bassi Wayahudi wakanena, Je! atajiua, kwa kuwa anena, Niendako mimi hamwezi kuja?

23 Akawaambia, Ninyi wa chini, mimi wa juu; ninyi wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.

24 Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.

25 Bassi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Neno lilo hilo nisemalo nanyi tangu mwanzo.

26 Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.

27 Hawakufahamu ya kuwa awatajia Baba.

28 Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.

29 Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo.

30 Alipokuwa akisema haya, wengi walimwamini.

31 Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;

32 tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru.

33 Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru?

34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambieni, Killa atendae dhambi, ni mtumwa wa dhambi.

35 Na mtumwa hakai ndani ya nyumba siku zote; mwana hukaa siku zote.

36 Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

37 Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.

38 Niliyoyaona kwa Baba yangu udiyo niyanenayo: nanyi vivyo hivyo mliyoyaona kwa baba yenu, ndiyo myatendayo.

39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ni Ibrahimu. Yesu akawaambia, Kama mugekuwa watoto wa Ibrahimu, mngetenda kazi zake Ibrahimu.

40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu.

41 Wakamwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zina; tuna baba mmoja, yaani Mungu.

42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.

43 Mbona hamyafahamu maneno yangu haya niyasemayo? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia neno langu.

44 Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.

45 Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini.

46 Nani wenu anishuhudiae kuwa nina dhambi? Nikisema kweli, mbona ninyi hamniamini?

47 Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.

48 Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?

49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.

50 Nami siutafuti ntukufu wangu; yuko atafutae na kuhukumu.

51 Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.

52 Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, nae amekufa? Na manabii wamekufa; wajifanya kuwa nani?

54 Yesu akajibu, Nikijitukuza nafsi yangu, utukufu wangu si kitu; anitukuzae ni Baba yangu; mmnenae ninyi kuwa ni Mungu wenu.

55 Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika.

56 Ibrahimu baba yemi alishangilia apate kuiona siku yangu; akaona, akafurahi.

57 Bassi Wayahudi wakamwambia. Hujapata bado miaka khamsini, na Ibrahimu umemwona?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo.

59 Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo