Yohana 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. 2 Na siku kuu ya Wayahudi, siku kuu ya vibanda, ilikuwa karibu. 3 Bassi ndugu lake wakamwambia, Ondoka bapa uende Yahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. 4 Kwa maana hakuna mtu afanyae neno kwa siri, na yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya haya, jidhihirishe kwa ulimwengu. 5 Maana hatta ndugu zake hawakumwamini. 6 Bassi Yesu akawaambia, Haujafika wakati wangu; wakati wenu sikuzote u tayari. 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 8 Pandeni ninyi kwenda kushika siku kuu hii; mimi sipandi bado kwenda kushika siku kuu hii: kwa kuwa wakati wangu haujatimia bado. 9 Alipokwisha kuwaambia haya, akakaa katika Galilaya. 10 Hatta ndugu zake walipokwisha kupanda, ndipo yeye nae akapanda kwenda kuishika siku kuu, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. 11 Bassi Wayahudi wakamtafuta katika siku kuu wakanena, Yuko wapi huyo? 12 Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano. 13 Illakini hapana mtu aliyemtaja kwa wazi kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. 14 Hatta ilipokuwa katikati ya siku kuu Yesu akapanda, akaingia hekalui akafundisha. 15 Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma? 16 Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka. 17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 18 Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu. 19 Aliyewapeni torati si Musa? wala hapana mmoja wenu aitendae torati. Mbona mnatafuta kuniua? 20 Makutano wakajibu, wakasema, Una pepo; ni nani anaetafuta kukuua? 21 Yesu akajibu, akawaambia, Nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnastaajabu. 22 Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. 23 Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24 Msihukumu hukumu ya macho, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. 25 Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua? 26 Na kumbe! ananena waziwazi wala hawamwambii neno? Yumkini wakuhwa wanajua kwa hakika ya kuwa huyu ni Kristo! 27 Lakini huyu twamjua atokako, bali Masihi atakapokuja, hakuna ajuae atokako. 28 Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 29 Lakini mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, nae ndiye aliyenituma. 30 Bassi wakatafuta kumkamata: lakini hapana aliyenyosha mkono wake illi kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. 31 Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? 32 Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate. 33 Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. 34 Mtanitafuta, wala hamtaniona; nami nilipo, ninyi hamwezi kuja. 35 Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani? 36 Neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; na nilipo mimi, ninyi hamwezi kuja? 37 Hatta siku ya mwisho, siku ile kubwa ya siku kuu, Yesu akasimama, akapaaza sauti yake, akinena, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni. 39 Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa. 40 Bassi watu wengi katika makutano waliposikia neno lile, walinena, Huyu hakika yake ndiye nabii yule. 41 Wengine walinena, Je! Kristo atoka Galilaya? 42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daud, na kutoka Bethlehemu, kijiji kile alichokaa Daud? 43 Bassi yakaingia matangukano kwa ajili yake. 44 Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hapana mtu aliyenyosha mkono wake illi kumshika. 45 Bassi wale watumishi wakawaendea makuhani wakuu na Mafarisayo, nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46 Wale watumishi wakajibu, Hajanena kamwe mwana Adamu aliye yote kama huyu anavyonena. 47 Bassi Mafarisayo wakawajibu, Je! ninyi nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo? 49 Lakini makutano hayo wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50 Akawaambia Nikodemo (ni yule aliyemwendea usiku, maana ni mmojawapo wao), 51 Je! sharia yetu humhukumti mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua atendavyo? 52 Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii. 53 Wakaenda killa mtu nyumbani kwake: |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania