Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI Bwana alipojua ya kuwa Mafarisayo wamesikia kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kubatiza,

2 (lakini Yesu mwenyewe hakuhatiza, hali wanafunzi wake),

3 akaacha Yahudi akaenda zake Galilaya marra ya pili.

4 Na alikuwa hana buddi kupita katikati ya Samaria.

5 Bassi akafika mji wa Samaria, uitwao Sukar, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusuf mwanawe.

6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Bassi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Ilikuwa yapata saa sita.

7 Akaja mwanamke wa Kisamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.

8 Maana wanafunzi wake wamekwenda mjini wanunue chakula.

9 Bassi yule mwanamke wa Kisamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke wa Kisamaria? kwa maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.

10 Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.

11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?

12 Je! wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki, nae mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na nyama zake?

13 Yesu akajibu, akamwambia, Killa anywae maji haya ataona kiu tena:

14 walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.

15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, nipe maji hayo, nisione kiu wala nisije huku kuteka.

16 Yesu akamwambia, Enenda, kamwite mume wako uje nae hapa.

17 Yule mwanamke akajibu akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume,

18 kwa maana umekuwa na waume watano, na yeye uliye nae sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.

19 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii.

20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, na ninyi husema kwamba Yerusalemi ni mahali patupasapo kuabudia.

21 Yesu akamwambia, Ee mwanamke, uniamini, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala katika Yerusalemi.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho: kwa kuwa wokofu watoka kwa Wayahudi.

23 Lakini saa inakuja, na sasa ipo, ambayo wenye ibada khalisi watamwabudu Baba katika roho na kweli: kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

24 Mungu ni roho, nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi (aitwae Kristo). Atakapokuja yeye, atatufunulia yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi nisemae nawe, ndiye.

27 Marra hiyo wakaja wanafunzi wake wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hapana aliyesema, Unatafuta nini? au, Kwa nini unasema nae?

28 Bassi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu,

29 Njoni, nitazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?

30 Bassi wakatoka mjini wakamwendea.

31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabbi, ule.

32 Akawaambia, Mimi nina chakula msichokijua ninyi.

33 Bassi wanafunzi wake wakasemezana, Je! mtu amemletea chakula?

34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.

35 Hamsemi ninyi, Imebaki miezi mine bado, ndipo yaja mavuno? Nami nawaambieni, Inueni macho yenu, mkayatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe tayari kwa mavuno.

36 Avunae hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, illi yeye apandae na yeye avunae wafurahi pamoja.

37 Maana neno lile, Mmoja hupanda, mwingine akavuna, huwa kweli.

38 Mimi naliwatuma myavune msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.

39 Na katika mji ule Wasamaria wengi wakaamini kwa sababu ya maneno ya yule mwananike, aliposhuhudu, kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda.

40 Bassi wale Wasamaria walipomwendea walimsihi akae kwao; akakaa huko siku mbili.

41 Watu wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.

42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako; maana tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika yake huyu ni Mwokozi wa ulimwengu.

43 Baada ya siku hizo mbili akaondoka huko, akaenda Galilaya.

44 Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudu ya kwamba nabii hana heshima katika inchi yake mwenyewe.

45 Bassi alipofika Galilaya Wagalilaya wakampokea, kwa kuwa wameona mambo yote aliyoyatenda Yerusalemi wakati wa siku kuu; maana hao nao waliendea siku kuu.

46 Bassi akafika tena Kana ya Galilaya, hapo alipofanya maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja, ana mwana hawezi Kapernaum.

47 Huyu aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yahudi hatta Galilaya, akamwendea, akamsihi ashuke akamponye mwana wake; kwa maana alikuwa kufani.

48 Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa.

49 Yule diwani akamwambia, Bwana, shuka kabla hajafa mtoto wangu.

50 Yesu akamwambia, Shika njia yako: mwana wako yu hayi. Mtu yule akaliamini lile neno aliloambiwa na Yesu, akashika njia.

51 Hatta alipokuwa akishuka, watumishi wake wakamlaki, wakampasha khabari, wakisema ya kama, Mtoto wako yu hayi.

52 Bassi akawauliza khabari ya saa alipoanza kuwa hajambo. Bassi wakamwamhia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.

53 Bassi baba yake akafahamu ya kuwa ni saa ileile aliyoambiwa na Yesu, Mwana wako yu hayi. Akaamini yeye na nyumba yake yote.

54 Na hii ni isharaya pili aliyoifanya Yesu, alipotoka Yahudi kwenda Galilaya.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo