Yohana 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 PALIKUWA na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi; 2 huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae. 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo amwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mama yake marra ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usitaajahu kwa kuwa nilikuambia, Hamna buddi kuzaliwa marra ya pili. 8 Upepo huenda utakako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na killa mtu aliyezaliwa kwa Roho. 9 Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa haya? 10 Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu? 11 Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali. 12 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamwa, mini, mtaaminije, niwaambiapo mambo ya mbinguni? 13 Na hapana mtu aliyepanda mbinguni, illa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu alioko mbinguni. 14 Na kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana buddi kuinuliwa: 15 illi asipotee mtu aliye yole amwaminiye, bali awe na uzima wa milele. 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae. 18 Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, watu wakapenda giza zaidi ya nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 20 Maana killa atendae manyonge huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasikemewe; 21 hali aitendae kweli huja kwenye nuru, matendo yake yaonekane ya kuwa yametendwa katika Mungu. 22 Baada ya haya Yesu na wanafunzi wake walikwenda hatta inchi ya Kiyahudi; akashinda huko pamoja nao, akibatiza. 23 Yohana nae alikuwa akibatiza huko Ainon, karibu na Salim, kwa sababu palikuwa na maji tele; watu wakamwendea wakabatizwa. 24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani. 25 Bassi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Wayahudi katika khabari ya utakaso. 26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabbi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ngʼambu ya Yardani, uliyemshuhudia wewe, huyu nae anabatiza, na watu wote wanamwendea. 27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. 28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. 29 Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia. 30 Yeye hana buddi kuzidi, bali mimi kupungua. 31 Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote. 32 Aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoshuhudia, wala hapana anaeukubali ushuhuda wake. 33 Aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri yake kwamba Mungu ni kweli. 34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima. 35 Baba ampenda Mwana, amempa vyote mikononi mwake. 36 Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania