Yohana 19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI ndipo Pilato akamtwaa Yesu, akampiga mijeledi. 2 Askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi jekundu; wakawa wakimwendea, 3 wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! wakimpiga makofi. 4 Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake. 5 Bassi Yesu akatoka nje, amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi jekundu. Pilato akawaambia, Tazama, Mtu huyu! 6 Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake. 7 Wayahudi wakamjibu, Sisi tuna sharia, na kwa sharia hiyo amepasiwa kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu. 8 Bassi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa; 9 akaingia tena Praitorio, akamwamhia Yesu, Umetoka wapi wewe? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10 Bassi Pilato akamwambia, Husemi na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukusulibisha na nina mamlaka ya kukufungua? 11 Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. 12 Tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si mpenda Kaisari; killa ajifanyae kuwa mfalme amfitini Kaisari. 13 Bassi Pilato, aliposikia maneno haya, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti, mahali paitwapo Sakafu ya mawe, na kwa Kiebrania Gabbatha. 14 Ilikuwa Maandalio ya Pasaka: ilikuwa panapo saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, mfalme wenu! 15 Bassi wale wakapiga kelele, Mwondoshe, mwondoshe, msulibishe. Pilato akawaambia, Nimsulibishe mfalme wenu? Makuhani wakuu wakajibu, Hatuna mfalme illa Kaisari. 16 Bassi ndipo akamtia mikononi mwao asulibishwe. Bassi wakampokea Yesu: 17 akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha; 18 wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja nae, huko na huko, na Yesu katikati. 19 Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. 20 Bassi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali paie aliposulihiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. 21 Bassi makuhani wakuu wa Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; hali ya kwamba yule alisema, Mimi mfalme wa Wayahudi. 22 Pilato akajihu, Niliyoandika nimeyaandika. 23 Bassi askari, walipomsulibisha Yesu, wakatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu mane, kwa killa askari fungu lake; nayo kanzu: na kanzu ile haikushonwa, imefumwa pia tangu juu. 24 Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari. 25 Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. 26 Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako. 27 Baadae akamwambia mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua kwake. 28 Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu. 29 Kikawako chombo kimejaa siki; bassi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya husopo, wakampelekea kinywani. 30 Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho. 31 Bassi Wayahudi, kwa maana ni Maandalio, miili isikae juu va msalaba siku ya sabato (maana siku ya sabato ile ilikuwa siku kuhwa), wakamwomba Pilato, miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. 32 Bassi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili aliyesulibiwa pamoja nae. 33 Walipomjia Yesu, wakiona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; 34 lakini askari mmoja kwa mkuki alimchoma ubavu, ikatoka marra damu na maji. 35 Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini. 36 Kwa maana haya yalitukia andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena, 37 andiko la pili lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. 38 Hatta baada ya haya, Yusuf, aliye wa Arimathaya, nae vu mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri (maana aliwaogopa Wayahudi), akamwomba Pilato rukhusa auondoe mwili wake Yesu: Pilato akampa rukhusa. Bassi akaenda akauondoa mwili wake. 39 Akaenda Nikodemo nae, yule aliyemwendea usiku hapo kwanza, akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia. 40 Bassi wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga saanda ya bafta, pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. 41 Na mahali pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani kaburi jipya, bado hajatiwa mtu aliye yote ndani yake. 42 Humo bassi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania