Yohana 18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 ALIPOKWISHA kusema haya, Yesu akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ngʼambu ya kijiti Kedron, palipo bustani; akaingia, yeye na wanafunzi wake. 2 Yuda nae, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikwenda huko marra nyingi pamoja na wanafunzi wake. 3 Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha. 4 Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti. 5 Yesu akawaambia, Mimi ndiye. Yuda nae aliyemsaiiti alikuwa akisimama pamoja nao. 6 Bassi alipowaambia. Mimi ndiye, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni kwaniba mimi ndiye; bassi mkinitafuta mimi, waacheni hawa waende zao; 9 illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao. 10 Bassi Simon Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu akamkata sikio lake la kuume. Na yule mtumishi jina lake alikwitwa Malko. 11 Bassi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga wako alani mwake. Kikombe alichonipa Baba, nisikinywee? 12 Bassi kile kikosi na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi wakamkamata Yesu, wakanifunga, 13 wakamchukua kwa Anna kwanza: maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule. 14 Na Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. 15 Simon Petro akamfuata Yesu, na mwanafunzi mwingine: na yule mwanafunzi alikuwa anajulika na kuhani mkuu: akaingia pamoja na Yesu behewani mwa kuhani mkuu; lakini Petro akasimama nje mlangoni. 16 Bassi yule mwanafunzi mwingine aliyejulika na kuhani mkuu akatoka akasema na mwanamke aliye mngoje mlango, akamleta Petro ndani. 17 Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi. 18 Na wale watumishi na askari walikuwa wamesimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi, wakawa wakikota moto. Petro nae, alikuwa pamoja nao, anakota moto. 19 Bassi kuhani mkuu akamwuliza Yesu khabari za wanafunzi wake, na khabari za mafundisho yake. 20 Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno. 21 Ya nini kumuliza? waulize wale waliosikia, ni nini niliyosema nao: wao wanajua niliyowaambia. 22 Aliposema maneno haya, mmoja wa wale watumishi aliyesimama karibu akampiga Yesu koli, akinena, Wamjibu hivi kuhani mkuu? 23 Yesu akamjibu, Kama nimesema mabaya, yashuhudie yale mabaya; bali kama nimesema mema, wanipigia nini? 24 Bassi Anna akampeleka amefungwa kwa Kayafa kuhani mkuu. 25 Na Simon alikuwa akisimama, anakola moto. Bassi wakamwambia, Wewe nawe je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake? Yeye akanena, Sio mimi. 26 Mmoja wa wale watumishi wa kuhani mkuu, ni jamaa yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Mimi sikukuona bustanini pamoja nae? 27 Bassi Petro akakana tena, jogoo akawika marra. 28 Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka. 29 Bassi Pilato akawatokea nje akasema, Mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? 30 Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtu mwovu, tusingemleta kwako. 31 Bassi Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa sharia yenu. Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna rukhusa kuua mtu; 32 illi neno lake Yesu litimizwe, alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa. 33 Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? 34 Yesu akajibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, ama watu wengine walikuambia khabari zangu? 35 Pilato akajibu, Je! mimi Myahudi? Taifa lako na makuhani wakuu ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu: watumishi wangu wangalinipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa. 37 Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu. 38 Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake. 39 Lakini kwenu kuna desturi, ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka: bassi, wapenda niwafungulie mfalme wa Wayahudi? 40 Bassi wakapiga kelele marra ya pili, wote pia, wakinena, Si huyu, bali Barabba. Nae Barabba alikuwa mnyangʼanyi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania