Yohana 17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe; 2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele. 3 Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza. 5 Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu. 6 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika. 7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako: 8 kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma. 9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako. 10 Na yote yaliyo yangu ni yako, na yaliyo yako ni yangu: nami nimetukuzwa ndani yao. 11 Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi. 12 Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa. 13 Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 Siombi uwatoe katika ulimwengu, hali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisiyvo wa ulimwengu. 17 Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli. 18 Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli. 20 Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma. 22 Nami, utukufu ule ulionipa nimewajia wao, wawe umoja, kama sisi tulivyo umoja: 23 mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24 Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania