Yohana 16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 MANENO haya nimewaambieni msije mkachukizwa. 2 Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada. 3 Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4 Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi. 5 Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi? 6 Illa kwa sababa nimewaambieni haya, huzimi imejaa mioyoni mwenu. 7 Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu; 9 Kiva khabari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10 kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11 kwa khabari ya hukumu, kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amehukumiwa. 12 Hatta ninayo mengi bado ya kuwaambieni, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 13 Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi: kwa kuwa atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari. 15 Yote aliyo nayo Baba m yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari. 16 Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba. 17 Bassi baadhi ya wanafunzi wake walisemezana, Neno gani hili analosema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo na mtaniona? na, Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba? 18 Bassi walisema. Neno gani hili analosema, hili Bado kitambo? Hatujui asemalo. 19 Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona? 20 Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mtalia, na kuomboleza, bali, ulimwengu utafurahi: ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha, 21 Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imekuja; hatta, akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena shidda, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22 Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae. 23 Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni. 24 Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu. 25 Haya nimesema nanyi kwa methali: saa inakuja, sitasema nanyi tena kwa methali, lakini nitawapa kwa wazi khabari ya Baba. 26 Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba; 27 kwa maana Baba mwenyewe awapenda ninyi, kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, mkaamini ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28 Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba. 29 Wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni methali yo yote. 30 Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31 Yesu akawajihu, Sasa hivi mnaamini? 32 Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania