Yohana 15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 MIMI ndimi niliye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ni mkulima. 2 Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisba kuwa safi kwa sababu ya neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea. 7 Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa. 8 Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama Baba alivyonipenda mimi, nami nimewapenda ninyi; kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake. 11 Haya nimewaambieni, illi furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 12 Amri yangu ndio hii, mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakima aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuweka uzima wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni. 16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni. 17 Haya nawaamuru, mpate kupendana. 18 Ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20 Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu. 21 Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka. 22 Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao. 23 Anichukiae mimi, humchukia na Baba yangu. 24 Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. 25 Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre. 26 Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27 Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania