Yohana 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo. 2 Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti, 3 bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu, 4 akaondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifungia. 5 Kiisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu yao, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifungia. 6 Bassi akafika kwa Simon Petro. Huyu akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyayo mimi, wewe huyafahamu sasa; lakini utayajua baadae. 8 Petro akamwambia. Hutanitawadha miguu milele. Yesu akamwambia, Nisipokutawadha, huna fungu pamoja nami. 9 Simon Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hatta mikono yangu na kichwa changu pia. 10 Yesu akamwambia, Aliyekwisha kuoga hana haja illa ya kunawa miguu, hali yu safi mwili wote; na ninyi m safi, lakini si nyote. 11 Maana alimjua atakaemsaliti, ndio maana alisema, Hamwi safi nyote. 12 Bassi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Mmeelewa niliyowatendea. 13 Ninyi mwaniita Mwalimu, na Bwana; na mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Bassi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa ninyi nanyi kutawadhana miguu. 15 Kwa kuwa nimewapeni mfano illi hayo niliyowatendea ninyi, na ninyi mtende yayo hayo. 16 Amin, amin, nawaambieni, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake: wala mtume si mkuu kuliko yeye aiiyempeleka. 17 Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda. 18 Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu. 19 Tangu sasa nawaambieni kabla hayajatukia, illi yatakapotukia, mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye. 20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka. 21 Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. 22 Wanafunzi wakatazamana, wakiona mashaka, ni nani anaemtaja, 23 Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda. 24 Bassi Simon Petro akampungia mkono huyo, amwulize, Ni nani anaemtaja? 25 Bassi yeye akimwegamia Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani? 26 Bassi Yesu akajibu, Ni mtu yule nitakaemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akampa Yuda, mwana wa Simon Iskariote. 27 Na baada ya lile tonge, Shetani akamwingia. Bassi Yesu akamwambia, Uyatendayo, yatende upesi. 28 Wala hapana mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu hatta akamwambia hivi. 29 Maana wengine, kwa kuwa Yuda aliuchukua mfuko, walidhani ya kuwa Yesu alimwambia, Nunua tunavyovihitaji kwa siku kuu; au kwamba awape maskini kitu. 30 Bassi huyu, akiisha kupokea lile tonge, akatoka marra hiyo; na ulikuwa usiku hapo alipotoka. 31 Bassi huyo alipokwisha kutoka, Yesu akanena, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, na Mungu ametukuzwa ndani yake: 32 Mungu akiwa ametukuzwa ndani yake, Mungu nae atamtukuza ndani ya nafsi yake; na marra atamtukuza. 33 Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi. 34 Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Hivi watu wote watajua ya kuwa m wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 36 Simon Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako, huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadae. 37 Petro akamwambia, Bwana, kwa nini nisiweze kukufuata sasa? Nitauweka uzima wangu kwa ajili yako. 38 Yesu akamjibu, Je! uzima wako utauweka kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hatta utakapokuwa umenikana marra tatu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania