Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI Yesu siku sita kabla ya Pasaka akafika Bethania, hapo alipokuwapo Lazaro, yule aliyekufa akaihfuliwa nae.

2 Bassi wakamfanyizia karamu huko; Martha akakhudumu. Na Lazaro alikuwa mmoja wa wale walioketi chakulani pamoja nae.

3 Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu.

4 Bassi Yuda Iskariote, mwana wa Simon, mmoja wa wanafunzi wake, aliye tayari kumsaliti, akanena,

5 Mbona marhamu haya hayakuuzwa kwa dinari mia tatu, na kupewa maskini?

6 Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.

7 Bassi Yesu alisema, Mwache, ameyaweka haya kwa siku ya maziko yangu.

8 Maana maskini mnao siku zote pamoja nauyi; bali mimi hamnami siku zote.

9 Bassi kundi kubwa la Wayuhudi walijua ya kuwa yeye yuko huko; wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, bali wamwone na Lazaro, ambae alimfufua katika wafu.

10 Makuhani wakuu wakafanya shauri wamwue Lazaro nae;

11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walikwenda zao, wakamwamini Yesu.

12 Siku ya pili watu wengi walioijia siku kuu, waliposikia kwamba Yesu anakuja Yerusalemi,

13 wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli.

14 Yesu akapata mwana punda, akampanda, kama ilivyoandikwa,

15 Usiogope, binti Sayuni: angalia, Mfalme wako anakuja, ameketi juu ya mwana wa punda.

16 Mambo haya wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walikumbuka ya kwamba ameandikiwa haya na ya kwamba walimtendea haya.

17 Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua.

18 Kwa sababu hiyo makutano wakaenda kumlaki, kwa sababu wamesikia ya kwamba amefanya ishara hii.

19 Bassi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno: tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.

20 Na palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliopanda kwenda kuabudu wakati wa siku kuu.

21 Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.

22 Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kiisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.

23 Yesu akajibu, akinena, Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu.

24 Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

25 Aipendae roho yake ataiangamiza; nae aichukiae roho yake katika ulimwengu huu ataihifadhi hatta uzima wa milele.

26 Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

27 Sasa roho yangu imefadhaika; niseme nini? Baba, uniokoe na saa hii. Lakini kwa ajili ya hayo naliifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako.

28 Bassi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

29 Bassi makutano waliosimama karibu wakasikia, wakanena kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema nae.

30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hii haikuwa kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.

31 Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu him atatupwa nje.

32 Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.

33 Alinena haya, illi kuonyesha ni mauti gani atakayokufa.

34 Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

35 Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.

36 Maadam mnayo nuru, iaminini nuru, mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake akajificha nao.

37 Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini;

38 illi litimizwe lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, nani aliyeziamini khabari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

39 Kwa sababu hii hawakuweza kuamini, kwa sababu Isaya alisema tena,

40 Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya.

41 Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake.

42 Walakini hatta katika wakubwa wengi walimwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumwungama, wasije wakalolewa katika masunagogi.

43 Kwa maana waliupenda utukufu wa wana Adamu kuliko utukufu wa Mungu.

44 Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka.

45 Nae anitazamae mimi, amtazama yeye aliyenipeleka.

46 Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.

47 Na mtu akisikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.

48 Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

49 Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.

50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele: bassi haya ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo