Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mtu wa mji wa Mariamu na Martha dada yake.

2 Ni Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu yake kwa nywele zake, ambae ndugu yake Lazaro alikuwa hawezi.

3 Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi.

4 Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wake Mungu, illi Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

5 Nae Yesu alimpenda Martha na dada yake ua Lazaro.

6 Bassi aliposikia kwamba hawezi alikaa bado siku mbili mahali pale alipokuwapo.

7 Kiisha baada ya haya akawaambia wanafunzi wake, Twende Yahudi tena.

8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabbi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga mawe, nawe unakweuda huko tena?

9 Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10 Bali akienda usiku, hujikwaa, kwa sababu nuru haimo ndani yake.

11 Aliyasema haya: kiisha baada ya liaya akawaambia, Lazaro rafiki yetu amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.

12 Bassi wale wanafunzi wake wakamwambia, Bwana, kama amelala atapona.

13 Lakini Yesu amenena khabari za mauti yake: nao walidhani ya kuwa ananena khabari za kulala usiugizi.

14 Bassi hapo Yesu akawaambia kwa wazi, Lazaro amekufa.

15 Nami nafurahi kwa ajili yenn kwamba sikuwa huko, mpate kuamini: lakini na twende kwake.

16 Bassi Tomaso, aitwae Didumo, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twende na sisi, tufe pamoja nae.

17 Bassi alipofika Yesu, akamkuta amekwisha kuwa kaburini yapata siku nne.

18 Na Bethania ilikuwa karibu ya Yerusalemi, kadiri ya stadio khamstashara;

19 na watu wengi katika Wayahudi wamekuja kwa Martha na Mariamu, illi kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.

20 Bassi Martha, aliposikia kwamba Yesu anakuja, akaenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.

21 Bassi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.

22 Lakini hatta sasa najua ya kuwa vyovyote utakavyomwomba Mungu, Mungu atakupa.

23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.

24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.

25 Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi,

26 na killa mwenye uzima na kuniamini mimi hatakufa kabisa hatta milele. Je! waamini haya?

27 Akamwambia, Naam, Bwana; mimi nimeamini ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajae ulimwenguni.

28 Na alipokwisha kusema haya, akaenda zake, akamwita dada yake, Mariamu, kwa siri, akisema, Mwalimu yupo, anakuita.

29 Nae aliposikia, akaondoka upesi, akamwendea.

30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji, lakini alikuwa pale pale alipomlaki Martha.

31 Bassi wale Wayahudi waliokuwa pamoja nae nyumbani, wakimfariji, walipomwona Mariamu, jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, wakamfuata, wakidhani ya kuwa anakwenda kaburini illi alie huko.

32 Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.

33 Bassi, Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana nae wanalia, akaugua rohoni, akajifadhaisha nafsi yake,

34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo, utazame.

35 Yesu akatoka machozi.

36 Bassi Wayahudi wakanena, Angalieni jinsi alivyompenda.

37 Bali wengine walisema, Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?

38 Bassi Yesu akiugua tena nafsini mwake akatika kaburini. Nalo lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.

39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule mtu aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa: maana amekuwa mayiti siku nne.

40 Yesu akamwambia, Sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Bassi wakaliondoa lile jiwe.

41 Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.

43 Akiisha kusema haya, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, toka, njoo huku.

44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa saanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa kitambaa. Yesu akawaambia, Mfungueni, kamwacheni aende zake.

45 Bassi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu na kuyaona aliyoyafanya Yesu, wakamwamini.

46 Lakini baadhi yao wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.

47 Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.

48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini: na Warumi watakuja, wataondoa mahali petu na taifa letu.

49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule, akawaambia,

50 Ninyi hamjui neno lo lote, wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu hawa, wala lisiangamie taifa zima.

51 Na hili hakusema kwa nafsi yake, hali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lile;

52 wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.

53 Bassi tangu siku ile walifanya shauri wapate kumwua.

54 Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.

55 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; wengi wakapanda toka inchi yote pia kwenda Yerusalemi kabla ya Pasaka, illi wajitakase.

56 Bassi wakamtafuta Yesu, wakasemezana wao kwa wao, wakisimama katika hekalu, Mwaonaje? Haji kabisa siku kuu hii?

57 Na Makuhani na Mafarisayo wametoa amri ya kwamba, mtu akimjua alipo, alete khabari, wapate kumkamata.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo