Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AMIN, amin, nawaambieni, asiyeingia kwa mlango katika zizi la kondoo, lakini apanda penginepo, huyu ni mwizi na mnyangʼanyi.

2 Aingiae kwa mlango ni mchunga wa kondoo.

3 Bawabu humfungulia huyu, na kondoo humsikia sauti yake, nae huwaita kondoo zake kwa majina yao, huwapeleka nje.

4 Awatoapo nje kondoo zilizo zake, huwatangulia; na kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.

5 Mgeni hawatamfuata kabisa, hali watamkimbia, kwa maana hawaijui sauti ya wageni.

6 Methali hii Yesu aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.

7 Bassi Yesu aliwaamhia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi niliye mlango wa kondoo;

8 wote walionitangulia ni wezi na wanyangʼanyi: lakini kondoo hawakuwasikia.

9 Mimi ndimi niliye mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka, ataingia, atatoka, na atapata malisho.

10 Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele.

11 Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo.

12 Mtu wa mshahara, na asiye mchunga, ambae kondoo si mali yake, humwona mbwa wa mwitu anakuja, huziacha kondoo, hukimbia; na mbwa wa mwitu huziteka, huzitawanya.

13 Mtu wa mshahara hukimhia kwa kuwa ni mtu wa mshahara, wala hatii moyoni mambo ya kondoo.

14 Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua,

15 kama vile Baba anijuavyo, na mimi nimjuavyo Baba: na uzima wangu nauweka kwa ajili ya kondoo.

16 Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.

17 Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena.

18 Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.

19 Yakaingia tena matangukano katika Wayahudi, kwa ajili ya maneno haya.

20 Wengi wao wakasema, Ana pepo, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?

21 Wengine wakasema, Maneno haya siyo ya mtu mwenye pepo. Je! pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?

22 Bassi ilikuwa siku kuu ya kutabaruku huko Yerusalemi; ni wakati wa baridi.

23 Na Yesu alikuwa akitembea ndani ya hekalu, katika ukumbi wa Sulemani.

24 Bassi Wayahudi wakamzunguka, wakamwambia, Hatta lini utatuangaisha roho zetu? Kama wewe u Kristo, tuambie wazi wazi.

25 Yesu akawajibu, Naliwaambieni, nanyi hamwamini; kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu, ndizo zinazonishuhudia.

26 Lakini ninyi hamwamini kwa sababu hammo katika kondoo zangu, kama nilivyowaambieni.

27 Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata;

28 nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.

29 Baba yangu aliyenipa ni mkuu kuliko wote; wala hakuna awezae kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

30 Mimi na Baba yangu tu nmoja.

31 Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige.

32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?

33 Wayahudi wakamjibu wakinena, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe, uliye mwana Adamu, wajifanya nafsi yako u Mungu.

34 Yesu akawajibu, Haikuandikwa katika torati yenu, ya kama, Mimi nilisema, Ninyi m miungu?

35 Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka),

36 je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

37 Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;

38 lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.

39 Wakatafuta marra ya pili kumkamata: akatoka mikononi mwao.

40 Akaenda zake tena ngʼambu ya Yardani, hatta pahali ptile alipokuwa Yohana akihatiza hapo kwanza; akakaa huko. Watu wengi wakamwendea, wakanena,

41 Yohana hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyosema Yohana katika khabari zake huyu yalikuwa kweli.

42 Wengi wakamwamini huko.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo