Yakobo 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 HAYA bassi, enyi matajiri! lieni yowe kwa sababu ya mashaka yanayokujieni. 2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho. 4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, uliozuiliwa nanyi kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabaoth. 5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6 Mmemhukumu mwenye haki mkamwua: nae hashindani nanyi. 7 Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8 Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 9 Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. 10 Watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. 11 Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma. 12 Lakini zaidi ya yote, ndugu, msiape kiapo cho chote, kwa mbingu wala kwa inchi; bali ndio yenu iwe ndio, na sio yenu iwe sio, msije mkaangukia hukumu. 13 Mtu wa kwenn amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi. 14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa wakamwombee, wakimpaka mafuta kwa jina la Bwana. 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa. 16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 17 Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, inchi ikazaa matunda yake. 19 Ndugu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali ya kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 20 ajue va kuwa veve amrejezae mwenye dhambi, atoke katika njia ya upotovu, ataiokoa roho ya mtu yule na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania