Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yakobo 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?

2 Mwatamani, wala hanma kitu; mwana na kuona wivu, na hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi.

3 Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu.

4 Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.

5 Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu?

6 Lakini atupa sisi neema nyingi zaidi; kwa hiyo asema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemi wanyenyekevu.

7 Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.

8 Mkaribieni Mungu, nae atsiwakaribieni ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, kaisafisheni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9 Jihuzunisheni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu kugeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa hamu.

10 Jidhilini mbele za Bwana, nae atawakuzeni.

11 Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.

12 Mtoa sharia na mbukumu ni mmoja tu, awezae kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umbukumuye mwenzako?

13 Haya bassi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia mji fullani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; nanyi hamjui yatakayokuwa kesho.

14 Uzima wenu ni nini? Maana ninyi moshi uonekanao kwa kitambo, kiisha hutoweka.

15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hayi na kufanya hivi au hivi.

16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kwote kwa namna hii ni kubaya.

17 Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo