Yakobo 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 MSIWE waalimu wengi, ndugu zangu, mkijua ya kuwa tutapata hukumu kubwa zaidi. 2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. 3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, illi watutii, na twageuza mwili wao wote. 4 Kaziangalieni merikebu; ingawa ni kubwua namna gani, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote aazimuko kwenda yule aongozae. 5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, na hujivuna majivuno makuu. 6 Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum. 7 Maana killa aina ya nyama, na ya ndege, na ya nyama watambaao, na ya vitu vilivyo baharini vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wana Adamu. 8 Bali ulimi hapana mwana Adamu awezae kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wana Adamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, mambo haya hayapasi kuwa hivyo. 11 Je! chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? 12 Ndugu zangu, mtini waweza kuzaa mazeituni au mzabibu tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na niaji matamu. 13 Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. 14 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli. 15 Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani, 16 maana hapo palipo wivu na magomvi, ndipo palipo machafuko, na killa tendo la aibu. 17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki; 18 na tunda la baki hupandwa katika amani kwa wale wafanyao amani. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania