Yakobo 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu, 2 Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa imani yenu huleta saburi. 4 Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno. 5 Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa. 6 Illa aombe kwa imani, pasipo shaka lo lote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa kwa upepo, na kupeperushwa huko na huko. 7 Maana mtu yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana; 8 mtu wa nia mbili asitasita katika njia zake zote. 9 Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa; 10 na tajiri kwa kuwa ameshushwa: kwa maana kama ua la majani atatoweka. 11 Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; na lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo nae tajiri atanyauka katika njia zake. 12 Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 13 Mtu, ajarihiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu: maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 14 Lakini killa mmoja hujaribiwa akivutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe. 15 Khalafu ile tamaa ikiisha kuchuikua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. 16 Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi. 17 Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka. 18 Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake. 19 Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu; 20 kwa maana ghadhabu ya mwana Adamu haiitendi haki ya Mungu. 21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, kapokeeni kwa upole neno lililopandwa, liwezalo kuokoa roho zenu. 22 Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyu ni kama mtu anaejiangalia uso wake wa asili katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kiisha huendazake, marra akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake. 26 Mtu akidhani ya kuwa ana dini, nae hazuii ulimi wake kwa khatamu, akijidanganya moyo wake, dini yake mtu yule haifai. 27 Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania