Waroma 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NASEMA kweli katika Yesu Kristo, sisemi uwongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu, 2 ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. 3 Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; 4 ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao, 5 na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin. 6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka; maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. 7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaak wazao wako watakwitwa; 8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao. 9 Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. 10 Wala si hivyo tu, lakini Rebeka nae, akiisha kuchukua mimba kwa mmoja, nae ni Isaak baba yetu— 11 kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, 12 si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitae aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. 13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. 14 Tuseme nini bassi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! 15 Maana alimwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiae. 16 Bassi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakae, wala wa yule apigae mbio, bali wa yule arehemuye, yaani Mungu. 17 Kwa maana maandiko yasema na Farao, ya kama, Nilikusimamisha, illi niouyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika inchi yote. 18 Bassi, kama ni hivyo, atakae (kumrehemu) humrehemu, na atakae kumfanya mgumu humfanya mgumu. 19 Bassi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana nani aliyeshindana na kusudi lake? 20 La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi? 21 An mfinyangi je! bana nguvu juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kufanya chombo kimoja, kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22 Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; 23 tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu, 24 ndio sisi tulioitwa nae, si watu wa Wayahudi tu, illa watu wa mataifa pia, utasemaje? 25 Ni vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita wale kuwa watu wangu wasiokuwa watu wangu, Na yeye mpenzi wangu asiyekuwa mpenzi wangu. 26 Na itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo watakwitwa wana wa Mungu aliye hayi. 27 Isaya nae atoa santi yake juu ya Israeli, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa. 28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya inchi, akilimaliza na kulikata. 29 Na kama isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa Sabaoth asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora. 30 Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani; 31 bali Israeli wakiifuata sharia ya haki hawakuifikilia ile sharia. 32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwaazalo, 33 kama ilivyoandikwa, Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao: Na killa amwaminiye hataaibishwa. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania