Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HAMJUI, ndugu (maana nasema nao waijuao sharia), ya kuwa torati humtawala mtu maadam yu hayi.

2 Kwa maana mwauamke aliye na mume amefungwa na sharia kwa yule mume maadam yu hayi: bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sharia ya mume.

3 Bassi wakati awapo hayi mume wake, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Bali mume wake akifa, amekuwa huru, hafungwi na sharia hiyo, hatta yeye si mzinzi, ajapokuwa na mume mwingine.

4 Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda.

5 Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.

6 Bali sasa tumetolewa katika torati isitukhusu kitu, tumeilia hali ile iliyotupinga, tupate kutumika sisi katika hali mpya chini ya roho, si katika hali ya zamani, ya dini ya sharia iliyoandikwa.

7 Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanza ndani yangu killa namna ya tamaa. Kwa maana dhambi hila sharia ni kifu.

9 Na mimi nalikuwa hayi hapo kwanza hila sharia; illa ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, na mimi nikafa.

10 Nikaona ile amri iletayo uzima, ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.

11 Kwa maana dhambi, ikipata nafasi kwa iie amri, ilinidanganya, ikaniua kwayo.

12 Bassi torati ni takatifu na ile amri takatifu ua ya haki na wema.

13 Bassi je! Ile iliyo njema ilikuwa manti kwangu mimi? Hasha! hali dhambi, illi ionekane kuwa dhambi, ilinifanyizia mauti kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.

14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni, bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

15 Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; na lile nilichukialo nalitenda.

16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, nakiri ya kuwa sheria ile ni njema.

17 Bassi sasa si mimi nilitendalo, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu.

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema: kwa kuwa kutaka ni katika uwezo wangu, bali kutenda lililo jema sipati.

19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.

20 Bassi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nilitendae, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Bassi nimeona sharia hii ya kuwa nipendapo kutenda lililo jema, liapo lililo baya ni karibu nami.

22 Kwa maana naifurahia sharia ya Mungu kwa mtu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sharia nyingine inapiga vita na ile sharia ya akili zangu, na kunifanya mateka va ile sharia ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu mimi bin Adamu! nani atakaeniokoa na mwili huu wenye kunifisha.

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo