Waroma 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 TUSEME nini bass? Tudumu katika dhambi illi neema iwe nyingi zaidi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo, twalibatizwa katika mauti yake? 4 Bassi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tutembee katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama tulivyounganika nae katika mfano wa mauti yake, kadhalika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 7 kwa maana yeye aliyekufa ameachiliwa akawa mbali ya dhambi. 8 Lakini tukiwa twalikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja nae, 9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka hafi tena, mauti haimtawali tena. 10 Kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi marra moja; lakini kule kuishi kwake, amwishia Mungu. 11 Vivyo hivyo na ninyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na wahayi kwa Mungu katika Kristo Yesu. 12 Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake; 13 wala msitoe viungo vyenu kuwa silaha ya dhulumu kwa dhambi; bali jitoeni nafsi zenu sadaka kwa Mungu kama walio hayi baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. 14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema. 15 Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha! 16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki. 17 Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 18 na mlipokwisha kuandikwa huru mkawa mbali ya dhambi, mlifanywa watumwa wa haki. 19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali ya haki. 21 Faida gani bassi mliyopata siku zile kwa mambo haya mnayotahayarikia sasa? kwa maana mwisho wa mambo haya ni mauti. 22 Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania