Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini?

2 Kwa maana ikiwa Ibrahimu alipewa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu.

3 Maana maandiko yasemaje? Ibrabimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

4 Lakini kwa mtu afanyae kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa neema bali kuwa deni.

5 Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

6 Kama vile Daud aunenavyo ukheri wake mtu yule ambae Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo;

7 Wa kheri waliosamehewa maasi yao, Na waliosetiriwa dhambi zao.

8 Yu kheri mtu yule ambae Bwana hamhesabii dhambi.

9 Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.

10 Alihesabiwaje bassi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

11 Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;

12 na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa.

13 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.

14 Maana ikiwa wale wa sharia ndio warithi, imani imekuwa burre, na ahadi imebatilika.

15 Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.

16 Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,

17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.

18 Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako.

19 Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara.

20 Wala hakuionea shaka ahadi ya Mungu kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani yake, akimtukuza Mungu,

21 akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa haki.

23 Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake,

24 bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu,

25 aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo