Waroma 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. 2 Na twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. 3 Ee bin-Adamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? 4 Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba? 5 bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, 6 atakaemlipa killa mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7 wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele; 8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu; 9 mateso na shidda juu ya killa roho ya mwana Adamu atendae uovu, kwanza Myahudi na Myunani pia: 10 bali utukufu na heshima na amani kwa killa mtu atendae mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; 11 kwa maana hapana upendeleo kwa Mungu. 12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sharia watapotea pasipo sharia, na wote waliokosa, wakiwa na sharia, watahukumiwa kwa sharia. 13 Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki. 14 Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe: 15 hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana; 16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo. 17 Lakini wewe, ukiwa unakwitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu, 18 na kuyajua mapenzi yake na kuyatambua manibo yaliyo bora, umeelimishwa katika torati, 19 na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani, 20 mkufunzi wra wajiuga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati, 21 hassi wewe umfundishae mwiugine, je! hujifimdishi nafsi yako? Wewe nkhubiriye kwamha mtu asiibe, waiba mwenyewe? 22 Wewe usemae kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiae sanamu, wateka mahekidu? 23 Wewe ujisifuye katika torati, kwa kuiasi torati wamvunjia Mungu heshima? 24 Kwa maana jina la Mungu lanenwa unajisi katika mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa. 25 Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. 26 Bassi ikiwti yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! kutokutahiriwa kwake hakutahesahiwa kuwa kutahiriwa? 27 Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati? 28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; 29 hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania