Waroma 13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KILLA nafsi itumikie mamlaka makuu; kwa maana hapana mamlaka yasiyotoka kwa Mungu: na mamlaka yaliyopo yameamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka ashindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatii watu khofu kwa ajili ya matendo mema, bali kwa ajili ya matendo mabaya. Bassi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? 4 Fanya mema, utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga burre: ni mtumishi wa Mungu, amlipizae kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo lazima kutumika, si kwa sababu ya ghadhabu tu, illa na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena mwatoa kodi; kwa kuwa wao ni watumishi wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyohiyo. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru: astahiliye khofu, khofu; astahiliye heshima, heshima. 8 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendae mtu mwenzake ameitimiza sharia. 9 Maana ile, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishududu uwongo, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani wako kama nafsi yako. 10 Peudo halimfanyizii jirani neno baya; bassi pendo ndio utimilifu wa sharia. 11 Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini. 12 Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru. 13 Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania