Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.

2 Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.

4 Kwa maana kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, navyo viungo vyote havitendi kazi moja;

5 vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake.

6 Bassi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa khuduma, tuwemo katika khuduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.

9 Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

10 Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;

12 kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu;

13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.

14 Wabarikini wanaowafukuzeni; barikini, wala msilaani.

15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

16 Mwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Andaeni yaliyo mema machoni pa watu wote.

18 Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote.

19 Msijilipize kisasi, wapenzi, bali ipisheni ghadhabu; maana imeandikwa, Kisasi juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

20 Bassi adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivi, utampalia makaa ya moto kichwani pake.

21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo