Waroma 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin. 2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea asili. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele ya Mungu, 3 Bwana, wamewaua nabii zakowamezibomoa madhbabu zako, nami mmesalia peke yangu, nao wanatafuta roho yangu. 4 Lakini ile jawabu yamwanibiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baal. 5 Bassi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako maliaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu. 6 Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo. 7 Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu. 8 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hatta wasione, na masikio hatta wasisikie mpalla leo. 9 Na Daud asema, Meza yao iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao; 10 Macho yao yatiwe giza wasione, Ukawainamisbe mgongo wao siku zote. 11 Bassi nasema, Je! wamejikwaa hatta wameanguka kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokofu umewafikilia mataifa, illi wao watiwe wivu: 12 bassi ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa mataifa, je! si zaidi sana utimilifu wao? 13 Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu. 14 Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi vao. 15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa? 16 Tʼena malimbuko yakiwa matakatifu, vivyo hivyo na, donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo vivyo hivyo. 17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 18 usijisifu juu ya matawi; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuae shina bali shina likuchukualo wewe. 19 Bassi utasema, Matawi yalikatiwa illi nitiwe mimi. 20 Marra haba. Yalikatiwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune bali uogope; 21 kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. 22 Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. 23 Na hao pia, wasipokaa katika kulokuamini kwao, watatiwa, kwa maana Mungu aweza kuwatia temi. 24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, ukatiwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema; si zaidi sana wale walio wa asili watatiwa katika mzeituni wao wenyewe. 25 Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili; 26 na hivi Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Yeye aokoae atakuja kutoka Sayuni Atamtenga Yakobo na maasi yake, 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. 28 Bassi kwa khabari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu, bali kwa khabari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya haha zetu. 29 Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto. 30 Kwa maana kama ninyi zamani mlimwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kutokuamini kwao, 31 vivyo hivyo na hao wameasi sasa, illi kwa kurehemiwa kwenu wao nao wapate rehema. 32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote. 33 Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani! 34 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? 35 Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, nae atalipwa? 36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania