Waroma 10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NDUGU, nia njema ya moyo wangu, na dua yangu niombayo Mungu kwa ajili ya Waisraeli ndio bii, waokolewe. 2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana wivu kwa ajili ya Mungu, lakini hauna msingi wa maarifa. 3 Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, na wakitaka kuithubutisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. 4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki. 5 Kwa maana Musa aieleza haki itokayo kwa sharia, akiandika ya kuwa, Mtu afanyae haya ataishi kwa haya. 6 Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakaepanda mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini,) 7 au, Ni nani atakaeshuka kuzimuni? (yaani, ni kuleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) 8 Lakini yasemaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulikhubirilo; 9 kwa sababu, ukimkiri Kristo Yesu kwa kinywa chako, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua, utaokoka; 10 kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu. 11 Kwa maana andiko lanena, Killa amwaminiye hatatahayarika. 12 Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao; 13 kwa kuwa killa atakaemwita Bwana kwa Jina lake ataokoka. 14 Bassi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mkhubiri? 15 Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema. 16 Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu? 17 Bassi imani, chanzo chake ni kusikla; na kusikia kunakuja kwa neno la Mungu. 18 Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu. 19 Lakini nasema, Israeli hakufahamu? Hapo kwanza Musa anena, Nitawatieni moyo wa bidii kwa watu wasio taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhabisha. 20 Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. 21 Lakini kwa israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na ubishi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania