Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,

2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,

3 khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,

4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,

5 ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;

6 katika hawa na ninyi mmekuwa, mmeitwa na Yesu Kristo:

7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.

8 Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.

9 Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu

10 nikiomba nije kwenu sasa katika siku hizi hizi, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu:

11 kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;

12 yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.

13 Sipendi msiwe na khahari, ndugu zangu, ya kuwa marra nyingi nalikusudia kuja kwemi, nikazuiliwa hatta sasa, illi nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo navyo katika mataifi mengine.

14 Nawiwa na Wayunani na washenzi, nawiwa na wenye hekima na wajinga.

15 Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuikhubiri Injili hatta na kwenu ninyi muaokaa Rumi;

16 kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.

17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hatta imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.

18 Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.

19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.

20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekima tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, yanafahamika kwa viumbe vyake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake; wtisiwe na udhuru:

21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza:

22 wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika,

23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye ua uharibifu kwa mfano wa sura ya bin-Adamu aliye ua uharibifu, na ya nyama wenye mbawa, na ya nyama wenye miguu mine, na ya nyama watambaao.

24 Kwa ajili ya bayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hatta wakavunjiana heshima miili yao:

25 kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kwa uwongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaehimidiwa milele. Amin.

26 Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hatta wanawake wakahadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili:

27 wanaume vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume kwa wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;

29 wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa;

30 watu wti nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakahari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,

31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema,

32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao haya wamestahili mauti, wanafanya haya, wala si hivyotu, bali wakubaliana nao wayatendao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo