Wakolosai 4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni. 2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani, 3 mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, 4 illi niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. 5 Enendeni kwa hekima mbele vao walio nje, mkiukomboa wakati. 6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu. 7 Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; 8 ambae nimemtuma kwenu kwa sababu hiyo hiyo, ajue mambo yenu, akawafariji mioyo yenu; 9 pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku. 10 Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11 Na Yesu aitwae Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. 12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu. 13 Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili yao walio katika Laodikia, na kwa ajili yao walio katika Hieropoli. 14 Luka, yule tabibu mpendwa, awasalimu, na Dema. 15 Wasalimuni ndugu walio katika Laodikia, na Numfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. 16 Waraka hun ukiisha kusomwa kwenu, fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. 17 Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize. 18 Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania