Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Wakolosai 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.

2 Nieni yaliyo juu, siyo yaliyo katika inchi.

3 Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

4 Kristo atakapoonekana, aliye uzima wetu, ndipo na ninyi mtaonekana pamoja nae katika utukufu.

5 Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:

6 kwa ajili ya hayo ghadhabu ya Mungu huwafikia wana wa kuasi.

7 Katika hayo na ninyi mlitembea zamani, mlipoishi katika haya.

8 Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.

9 Msiambiane uwongo, kwa kuwa mmemvua mtu wa kale, pamoja na matendo yake,

10 mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.

11 Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.

12 Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

13 mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.

14 Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15 Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.

16 Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.

17 Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kania ipendezavyo katika Bwana.

19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, msiwe na uchungu nao.

20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jamlio hili lapendeza katika Bwana.

21 Ninyi haha, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

22 Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.

23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wana Adamu,

24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana njira wa urithi; kwa kuwa mnamtumikia Bwana Kristo.

25 Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo