Wafilipi 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KHATIMAE, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa niuyi. 2 Jihadharini na mbwa, jihadharini nao watendao mabaya, jihadharini nao wajikatao. 3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. 4 Mtu ye yote akijiona anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi. 5 Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa, 6 kwa jinsi ya haki ipatikanayo kwa sharia sikuwa na khatiya. 7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyaona kuwa khasara kwa ajili ya Kristo. 8 Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo; 9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 10 nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11 illi nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; illa natenda kitu kimoja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, 14 nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. 15 Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo. 16 Illakini, hapo tulipofika na tuenende kwa kanuni ile ile. 17 Mwe wafuasi wangu, ndugu, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliokupeni. 18 Maana wengi huenenda, nimewaambieni marra nyingi khabari zao, na hatta sasa nawaambieni kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; 19 mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani. 20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo; 21 atakaeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule awezao kuvitiisha hatta na vitu vyote chini yake. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania