Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Wafilipi 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;

2 Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.

3 Namshukuru Mungu wangu killa niwakumbukapo,

4 siku zote killa niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,

5 kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ya kwanza hatta leo hivi;

6 niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;

7 kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.

8 Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku katika moyo wake Kristo Yesu.

9 Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;

10 mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,

11 mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.

12 Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yamekuja yakaieneza Injili;

13 hatta vifungo vyaugu vimekuwa dhahiri katika Kristo, katika praitorio, na kwa wengine wote.

14 Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.

15 Wengine wanakhubiri khabari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina: na wengine kwa nia njema.

16 Hawa wanamkhubiri Kristo kwa fitina wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza taabu za kufungwa kwangu;

17 na hawa wengine kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa illi niitetee Injili.

18 Yadhuru nini? bali kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anakhubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.

19 Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo,

20 kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.

21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.

22 Illa ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; bassi nitakalolichagua sitambui.

23 Ninasongwa kati kati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo; maana ni vizuri zaidi;

24 bali kudumu katika mwili kwuhitajiwa zaidi kwa ajili yenu.

25 Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani;

26 kujisifu kwenu kupate kuzidi katika Kristo Yesu kwa ajili yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi nyote tena.

27 Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;

28 wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.

29 Maana mmepewii kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, illa na kuteswa kwa ajili yake,

30 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, mkasikia kvvamba ninayo hatta sasa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo