Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waefeso 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WATOTO, watiini wazazi wenn katika Bwana, maana hii ndio haki.

2 Waheshimu baba yako na mama yako (amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),

3 upate ukheri, nkakae sana katika dunia.

4 Na ninyi, akina baba, msiwachokoze watoto wemi; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

5 Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,

6 wala si kwa utumwa wa macho kama wajipendekezao kwa wana Adamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;

7 kwa nia njema mkimtumikia Bwana wala si mwana Adamu:

8 mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.

9 Na ninyi, akina bwana, watendeni yayo bayo, mkiacha kuwaogofya, mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, na kwake hapana upendeleo.

10 Ndugu zangu, mwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani.

12 Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kutimiza yote kusimama.

14 Simameni, bassi, mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa haki vifuani,

15 na kufungiwa miguu bali ya kuwa fayari tupatayo kwa Injili ya amani;

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chepeo ya wokofu, na upanga wa Roho, ndio neno la Mungu;

18 kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,

19 na mimi pia, nipewe usemi, kwa kufumhua kinywa changu kwa ujasiri, niikhubiri siri ya Injili,

20 kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema.

21 Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote;

22 ambae nilimpeleka kwenu kwa kusudi hili hili mpate kuyajua mambo yetu, nae akawafariji mioyo yenu.

23 Amani kwa ndugu, na pendo pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo.

24 Neema iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu pasipo hila. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo