Waefeso 5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI mwe wafuasi wa Mungu, kama watoto wanaopendwa; 2 mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri. 3 Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu; 4 wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi; haya hayapendezi; bali afadhali kushukuru. 5 Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi. 7 Bassi msishirikiane nao. 8 Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru; 9 (kwa kuwa tunda la nura ni katika wema wote na haki na kweli); 10 mkihakiki nini impendezayo Bwana. 11 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 12 kwa kuwa yanayotendeka nao kwa siri, ni aibu hatta kuyanena. 13 Lakini yote yakemewapo, hudhihirishwa na nuru; maana killa kitu kinachodhihirisha ni nuru. 14 Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza. 15 Angalieni sana, bassi, jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio hekima, bali kama wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati, kwa maana zamani bizi zina novu. 17 Kwa sababu hii msiwe wajinga, bali watu wanaofahamu nini mapenzi ya Bwana. 18 Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho; 19 mkisemezana kwa zaburi na fenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20 mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; 21 mkitumikiana katika khofu ya Kristo. 22 Ninyi wake, watumikieni waume zenu kama kumtumikia Bwana wetu. 23 Maana mume ni kichwa cha mke, kama nae Kristo ni kichwa cha kanisa; nae ni mwokozi wa mwili. 24 Kwa hivyo kama Kanisa limtumikiavyo Kristo, vivyo hivyo nao wake wawatumikie waume zao katika killa jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake, 26 kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendae mkewe hujipenda nafsi yake; 29 maana hakuna mtu anaechukia mwili wtike, bali huulisha na kuutunza, kama Bwana anavyolitendea Kanisa; 30 kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha haha yake na mama yake, ataamhatana na mkewe; nao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa. 33 Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania