Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waefeso 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA ninyi, mlipokmva wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zemi,

2 mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;

3 ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.

4 Lakini Mungu kwa kuwa mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda,

5 hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);

6 akatufufua pamoja nae, akatuketisha pamoja nae katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu:

7 illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.

8 Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:

9 wala si kwa matendo, asije mtu awae yote akajisifu.

10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.

11 Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:

12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza, mmekuwa karibu kwa damu ya Kristo.

14 Maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiyambaza cha kati kilichotutenga,

15 akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani;

16 na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;

17 akaja, akakhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na kwao waliokuwa karibu.

18 Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja.

19 Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,

20 mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;

21 katika yeye jengo lote likiungamanishwa vema linakua hatta liwe hekalu takatifu katika Bwana;

22 katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo