Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waefeso 1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;

2 Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo.

3 Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo;

4 kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo.

5 Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,

6 illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:

7 Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;

8 aliyotuzidishia katika hekima yote na ujuzi;

9 akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,

10 ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:

11 ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;

12 illi sisi tuwe sifa ya utukufu wake, tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu;

13 katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,

14 aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.

15 Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,

16 siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu;

17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:

18 macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,

19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari,

20 aliyotenda katika Kristo alipomfufua, akamweka mkono wake wa kuume katika mbingu,

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na killa jina litajwalo, si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao nao;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajiii ya kanisa,

23 lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo