Waebrania 9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI hatta agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidumia. 2 Maana khema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na taa, na meza, na mikate iliyotolewa kwa Mungu; palipoitwa, Patakatifu. 3 Na nyuma ya pazia la pili, ile khema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, 4 yenye cheteso cha dhahabu, na sanduku ya agano iliyofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye manna, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano; 5 na juu yake makerubi ya utakatifu, yakilitia kivuli kao la rehema; bassi hatuma nafasi ya kueleza khabari za vitu hivi moja moja. 6 Bassi, vitu hivi vikiislia kutengenezwa hivyo, makuhani huingia khema ya kwanza siku zote, wakiyatimiza mambo va ibada. 7 Lakini katika khema ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, marra moja killa mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na dhambi za ujinga za watu. 8 Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama. 9 Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake, 10 kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya. 11 Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. 13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ngʼombe waliyonyunyizwa wenye uchafu hutakasa hatta kuutakatisha mwili; 14 bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi? 15 Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. 16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, maadam yu hayi yeye aliyelifanya. 18 Kwa hiyo hatta lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. 19 Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, 20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. 21 Na ile khema na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivi hivi. 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. 23 Bassi sharti manukulu ya mambo yaliyo mbinguni yasafishwe kwa haya, lakini mambo ya mbinguni yenyewe kwa dhabibu zilizo bora kuliko haya. 24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; 25 wala si kusudi ajitoe marra nyiugi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo patakatifu killa mwaka kwa damu isiyo yake; 26 kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 27 Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu: 28 kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania