Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,

2 mkhudumu wa patakatifu, na wa khema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwana Adamu.

3 Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe.

4 Kama angekuwa juu ya inchi, asingekuwa kuliani; maana wapo watoapo sadaka kama iagizavyo sharia;

5 watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

6 Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.

8 Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililofanyana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao uiwatoe katika inchi ya Misri.

9 Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwaangalia, asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.

11 Nao hawatafundishana killa mtu na jirani yake, na killa mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watunijua, tangu mdogo wao hatta mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe dhumlumu zao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo