Waebrania 6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu, 2 na mafundisbo ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. 3 Na tutafanya hayo kama Mungu akitujalia. 4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. 7 Maana inchi iinywayo mvua iijiayo marra kwa marra, na kuzaa maboga yejiye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hupokea baraka kwa Mungu; 8 bali ikitoa miiba ua magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; mwisho wake ni kuteketea. 9 Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu: 10 maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia. 11 Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho; 12 illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu. 13 Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa kuwa alikuwa hana mkuhwa kuliko nafsi yake wa kumwapia, aliapa kwa nafsi yake, 14 akisema, iiakika yangu nitakubariki, na hakika yangu nitakuongeza. 15 Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. 16 Maana wana Adamu humwapia yeye aliye mkuu: na ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kiyathubutishe. 17 Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha wairithio ile ahadi jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; 18 illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; 19 tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia, 20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania