Waebrania 3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, 2 Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemfanya, kama Musa nae alivyokuwa katika nyumba yake yote. 3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kamti vile yeye aitengenezae nyumba alivyo na heshima zaidi ya nyumba hiyo. 4 Maana killa nyumba imetengenezwa na mtu; illa yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5 Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa; 6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho. 7 Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake, 8 msifanye migumu mioyo yenu, kama wakati wa kunikasirisha, siku ya kujaribiwa katika jangwa, 9 hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, wakaona matendo yangu miaka arubaini. 10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu; 11 kama nilivyoapa katika hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu. 12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi. 13 Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho; 15 hapo inenwapo, Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu kama wakati wa kunikasirisha. 16 Maana ni nani waliomkasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka katika Misri wakiongozwa na Musa? 17 Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? 18 Na ni nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, illa wale wasioamini? 19 Bassi twaona ya kuwa bawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania