Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.

2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

3 sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;

4 Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

5 Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena,

6 illa mtu mmoja ameshuhudu hivi maliali fullani, Mwana Adamu ni nini hatta umkumbuke, ama mwana wa binadamu hatta umwangalie?

7 Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemweka jua ya kazi za mikono yako;

8 nmetia vitu vyote chini ya uyayo zake. Kwa maana katika kutia vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichotiwa. Illakini sasa hado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake,

9 illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.

10 Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.

11 Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;

12 akinena, Nitalikhubiri jina lako kwa ndugu zangu; kati kati ya kanisa nitakuimba,

13 na tena, Nitamtumaini: na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.

14 Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,

15 akawaokoe wale ambao kwamba maisha zao zote kwa khofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.

16 Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, illa atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.

17 Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.

18 Na kwa kuwa aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo