Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, tuweke kando killa mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa uvumilivu katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2 tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyavumilia mapingamizi makuu namna hii ya wenye dhambi juu ya nafsi zao, msije mkadhoofika mkizimia mioyoni mwenu.

4 Hamjafanya vita kiasi cha kumwaga damu, mkishindana na dhambi:

5 tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama na wana. Mwanangu, usikudharau kurudi kwake Bwana, Wala, usizimie ukikemewa nae;

6 Maana yeye ambae Bwana humpenda, humrudi, Nae humpiga killa mwana amkubaliye.

7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwavumilia; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiorudiwa na baba yake.

8 Bassi kama mkiwa hamna kurudiwa walikoshiriki wote, mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

9 Na pamoja na haya tulikuwa na baba za mwili wetu walioturudi, tukawastahi; bassi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi.

10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu illi tuushiriki utakatifu wake.

11 Killa adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini huwatolea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,

13 mkaifanyia miguu yenu njia za kunyoka, illi kitu kilicho kilema kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

14 Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;

15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.

16 Asiwepo asharati au asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.

17 Maana mwajua ya kuwa hatta alipotaka baadae kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.

18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingi jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno;

19 ambayo wale waliosikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine; maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa,

20 Hatta nyama akiugusa mlima atapigwa mawe au atachomwa kwa mkuki.

21 Na baya yaliyoonekana yalikuwa ya kutisha, hatta Musa akasema, Nashikwa na khofu na kutetemeka.

22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.

25 Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:

26 Ambae sauti yake iliitemetesha inchi wakati ule: lakini sasa ameahidi akinena, Marra moja tena naitetemesha inchi wala si inchi tu, bali na mbingu pia.

27 Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

28 Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:

29 maana Mungu wetu ni moto ulao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

Bible Society of Tanzania
Tufuate:



Matangazo