Waebrania 11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 19211 BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 2 Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. 4 Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena. 5 Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. 6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. 7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. 8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9 Kwa imani alikaa katika ile inchi ya ahadi, kama katika inchi isiyo yake, akikaa katika khema pamoja na Isaak na Yakobo, warithi pamoja nae wa ahadi ile ile. 10 Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu. 11 Kwa imani hatta Sara mwenyewe alipokea nwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimwona yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. 12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, nae kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufukoni, usioweza kuhesabiwa. 13 Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi. 14 Maana wasemao maneno kama hayo waonyesha kwa wazi kwamba wanatafuta inchi yao wenyewe. 15 Na kama wangaliikumbuka inchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. 16 Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. 17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaak, awe dhabihu; na yeye aliyezipokea ahadi alikuwa akimtoa mwana wake, mzaliwa wake wa pekee; 18 naam, yeye aliyeamhiwa, Katika Isaak uzao walio utaitwa, 19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano. 20 Kwa imani Isaak akawahariki Yakobo na Esau, hatta katika khabari ya mambo yatakayokuwa baadae. 21 Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki killa mmoja wa wana wa Yusuf, akaabudu akiegemea kitanda chake. 22 Kwa imani Yusuf, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja khabari za kutoka kwao wana wa Israeli, akawaagizia mifupa yake. 23 Kwa imani Musa, alipozatiwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. 24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; 25 akaona ui afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa dhambi kitamho; 26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri. 27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana. 28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kunyunyiza ile damu, illi mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. 29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Sham, kama katika inchi kavu; Wamisri wakaijaribia wakatoswa. 30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zikiisha kuzungukwa siku saba. 31 Kwa imani Rahab, yule kahaba, hakuangamia pamoja nao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wapelelezi kwa amani. 32 Na niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta khabari za Gideon na Barak na Samson na Yeftha na Daud na Samwil na manabii; 33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, waliziba makanwa ya simba, 34 walizima nguvu za moto, waliokoka na ukali wa upanga. Walitiwa nguvu baada va kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. 35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa: na wengine walibanwa, wasiukubali ukombozi, wapate ufufuo ulio bora: 36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani: 37 walipigwa mawe, walikatwa kwa msumeno, walishawishwa, waliuawa kwa upanga: walizungukazunguka, wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; waiikuwa wahitaji, wakindhiwa, wakitendwa mabaya: 38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao): walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya inchi. 39 Na watu hawa wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi: 40 kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi. |
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Bible Society of Tanzania